NINI MAANA YA SABATO
Sabato (kwa Kiebrania: שבת, shabbāt, yaani pumziko kwa Kiswahili) ni siku ya pumziko ya kila juma katika Uyahudi kwa ujumla na hasa katika nchi ya Israeli. Neno hilo linaonekana kwa mara kwanza kwenye Biblia katika amri ambazo taifa la kale la Israeli lilipewa. (Kutoka 16:23).
Kulingana na Kutoka 20: 8–11, Sabato ni siku ya saba ya juma, ambayo tunapaswa kupumzika, kwa kukumbuka kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa siku sita na kisha "akapumzika" siku ya saba.
Sabato ndio kitu cha kwanza Mungu alichokiita kitakatifu – Mwanzo 2:2-3
Mungu aliiumba sabato kama zawadi kwa mwanadamu – Marko 2:27-28
Sabato ni mfano wa pumziko la milele – Waebrania 4:9-14
JE, TUMEAGIZWA KUFANYA NINI SIKU YA SABATO
Kuikumbuka, kuitunza, na kupumzika – Kutoka 20:8, Kumb 5:12, Kumb 5:14-15
BARAKA GANI ZINAPATIKANA KATIKA KUITUNZA SABATO
Kutokuharibiwa – Lawi 19:30-31
Kutokutawaliwa – 1 Korinto 6:12
Usalama/ulizi – lawi 33:12
