IFAHAMU ZAIDI IMANI YA MITUME

Je, wewe unafahamu nini kuhusiana na Imani ya Mitume (inayounganisha wakristo Ulimwenguni mwote) ambayo Wakristo wengi ulimwenguni huungana pamoja katika kuikiri? Katika makala hii tutajifunza kwa ufupi juu ya Imani ya Mitume. Ni matumaini yangu kuwa makala hii itakufungua angalau kidogo katika kuifahamu Imani ya Mitume, na kuungana na Wakristo wengine katika kuikiri.  Kanuni za Kiimani Tangu kuanzishwa kwa Kanisa, Wakristo walitengeneza miuhtasari mifupi na rahisi ya imani. Mihutasari hii mifupi ilijulikana kama hihtasari ama kanuni za imani. Mojawapo ya Mihtasari hii mifupi ni Imani ya Mitume. Watu walipokuwa wakijiandaa kwa ubatizo katika karne za mwanzo za Kanisa la Kikristo walijifunza muhtasari mfupi wa kile ambacho Wakristo wote walikiamini. Mojawapo ya mihtasari hii ya Imani ni Imani ya Mitume ambayo ilikubalika na kupokelewa kwa upana katika kanisa, kwasababu ilionekana kuwa na   mafundisho muhimu kutoka kwa wale mitume 12 waliokuwa wafuasi wa kwanza wa Yesu. Ilikuw...