IFAHAMU ZAIDI IMANI YA MITUME

Je, wewe unafahamu nini kuhusiana na Imani ya Mitume (inayounganisha wakristo Ulimwenguni mwote) ambayo Wakristo wengi ulimwenguni huungana pamoja katika kuikiri? Katika makala hii tutajifunza kwa ufupi juu ya Imani ya Mitume. Ni matumaini yangu kuwa makala hii itakufungua angalau kidogo katika kuifahamu Imani ya Mitume, na kuungana na Wakristo wengine katika kuikiri. 


Kanuni za Kiimani


Tangu kuanzishwa kwa Kanisa, Wakristo walitengeneza miuhtasari mifupi na rahisi ya imani. Mihutasari hii mifupi ilijulikana kama hihtasari ama kanuni za imani. Mojawapo ya Mihtasari hii mifupi ni Imani ya Mitume. Watu walipokuwa wakijiandaa kwa ubatizo katika karne za mwanzo za Kanisa la Kikristo walijifunza muhtasari mfupi wa kile ambacho Wakristo wote walikiamini. Mojawapo ya mihtasari hii ya Imani ni Imani ya Mitume ambayo ilikubalika na kupokelewa kwa upana katika kanisa, kwasababu ilionekana kuwa na  mafundisho muhimu kutoka kwa wale mitume 12 waliokuwa wafuasi wa kwanza wa Yesu. Ilikuwa ni katika imani ya mitume Wakristo walikiri kupokea ubatizo katika Kristo. Imani ya Mitume ni muhtasari wa kile Kanisa linafundisha, na kile ambacho Wakristo kwa pamoja wanaamini.


Imani ya Mitume


Namwamini Mungu Baba mwenyezi, muumba mbingu na nchi:


Na Yesu Kristo Mwana wake pekee, Bwana wetu, aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na bikira Mariamu, akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashuka mahali pa wafu; siku ya tatu akafufuka, akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba  Mwenyezi, kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na watu wafu.


Namwamini Roho Mtakatifu; na kanisa takatifu ya Waamini wote; na ushirika wa watakatifu; na ondoleo la dhambi; na kiyama ya mwili; na uzima wa milele.

Amina.


Chanzo cha Imani ya Mitume


Wakati fulani iliaminiwa na kufundishwa kwamba Imani ya Mitume iliandikwa katika kipindi cha karne ya kwanza na mitume kumi na wawili wenyewe. Hata hivyo iliaminika pia kuwa kila mtume alichangiwa wazo lake la kitheolojia katika maneno yaliyomo katika Imani ya Mitume. Lakini ukweli ni kwamba hakuna udhibitisho wala ushahidi wowote katika historia unaoonyesha kuwa Mitume walihusika kwa njia moja ama nyingine katika kuunda ama kuandaa Imani hii ya Mitume ambayo tunaungana na wakristo wote Ulimwenguni kuikiri. Kama mitume hawakuandika Imani hii ya mitume ni nani alihusika? Ni ngumu kusema ni nani aliandika kwa sababu hakuna mwandishi aliyejitokeza kudhibitisha kuwa yeye ndio mwandishi halali/halisi.


Wapo ambao waliamini kuwa Imani hii ya Mitume ilianza na maswali ambayo wakristo walikua wakiulizwa wakati wa kupata ubatizo au kukiri kile wanachokiamini. Mfano ‘unaamini katika Mungu Baba aliyeumba Mbingu na nchi? Je, unaamini kuwa Kristo alichukuliwa mimba kwa uweza wa Roho mtakatifu na kuzaliwa na bikira Maria’ nk.


Katika karne ya kwanza na ya pili, huenda ikawa kila kutaniko la kanisa lilikuwa na taratibu zake za kiimani, au njia ya kufupisha ukweli muhimu wa Biblia kwa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kusoma ama kuielewa Biblia kwa kina. Sio watu wote walikua na uwezo wa kuelewa ama kustaimili yale yaliyokuwa kwenye Biblia kwa kipindi kichyo. Lakini kufikia karne ya tatu au ya nne, misingi ama taratibu fulani za kiimani zilikuwa zikizidi kuwa maarufu zaidi na kutumika katika makanisa mengi.


Taratibu ama Imani mojawapo ambayo ilijivunia umaarufu kwa njia hii ilikuwa ni imani ya kanisa la Roma, Imani ambayo ilitambulika kwa jina la Imani ya Roma. Imani hii inafanana sana na Imani ya Mitume na ilipelekea wasomi wengi kuamini kuwa Imani ya Mitume ilikua ni toleo la baadaye baada ya Imani hii ya Roma. Ukweli ni kwamba Imani ya mitume haikutokana na Imani ya Roma, bali ilianzia katika kanisa la kwanza la Kristo.


Kusudi la kuundwa kwa Imani ya Mitume


Imani ya mitume iliundwa ili kuwawezesha wakristo kuwa waaminifu na neon la Mungu na kuendelea kusimama katika kweli ya Mungu na kuwa na umoja katika kanisa la Kristo Bwana wetu.  Iliundwa ili kuwasaidia watu kupata muhtasari wa Neno la Mungu na kuwa na uwezo wa haraka katika kuishika kweli ya Kristo na kuepuka udanganyifu ambao ungeweza kuingizwa katika kanisa na waalimu wa uongo.


Mkristo atambue nini katika neno la Mungu pamoja na Imani ya Mitume?


Kuwa wakati kwa nia njema tunaweza kuchukulia kanuni fulani za imani kuwa ni sawa na neno la Mungu (Biblia). Japo tunaikiri Imani ya Mitume, ni lazima kuelewa kuwa maandiko matakatifu ni neno la Kristo na ndilo lenye mamlaka juu ya vitu vingine vyote, na ndilo chanzo cha mafundisho yote ya kweli. Tusije tukalisahau neno la Kristo na kushikamana na tamaduni zetu ndani ya Kanisa. Hakuna tamaduni au imani inayopaswa kuinuliwa au kulinganishwa na neno la Mungu. Biblia pekee ndio chanzo na msingi wetu katika Imani. Tamaduni za Imani kama Imani ya Mitume ni zana ya kufundishia na kutoa muhtasari wa uelewa wetu wa Maandiko.


Imani ya Mitume inatusaidia vipi sisi Wakristo katika Imani yetu?


Kama tulivyoona, hakuna kanuni ama tamaduni ya imani inayoweza kuchukua nafasi ya Maandiko. Lakini hii haimaanishi kwamba kanuni ama taratibu za imani hazina nafasi katika maisha ya Kikristo. Imani ya Mitume ni zana inayotoa kanuni na taratibu kwa watu wa Mungu. Moja ya kazi muhimu ya Imani ya Mitume, kama kanuni zote za kiimani, ni kulisaidia kanisa katika kujua ukweli juu ya Mungu, kurekebisha mafundisho ya uongo ambayo yanaweza kuingizwa ndani ya kanisa, kufundisha na kuandaa waumini wapya kwa uaminifu na ukomavu katika imani ya kanisa. Pia inatuongoza na kutusaidia katika kumwabudu Mungu na kuikiri Imani, na zaidi ya yote ni kutoa muhtasari wa Imani ya Mkristo na kuliweka kanisa la Kristo katika umoja.


Imani ya Mitume inatukumbusha ukweli uliopo ndani ya imani yetu, kufafanua ufunuo wa Biblia juu ya Yesu Kristo, na kazi Kristo katika ukombozi wetu. Kanisa linategemea mukhtasari mfupi wa imani katika kuungama pamoja na kueneza Ukristo wa kweli ulimwenguni kote.


Hitimisho:


Katika haya tuliojifunza juu ya Imani ya Mitume, na wakati ulimwengu ukiendelea kuchanganikiwa na kuliacha neno la Mungu, ni muhimu kwa wakristo wote kusimama Imara katika Maandiko na kuijua kwa kina kweli ya Mungu ili kuepuka mafundisho na Imani za uongo ambazo zinaendelea kuzaliwa siku hadi siku. Mababa wa kanisa walielewa ukweli huu, ndiyo maana walifanya kazi kwa bidii ili kulitolea kanisa muhtasari wa uaminifu wa mafundisho ya Maandiko, kama Imani ya Mitume.


Kwasababu ya Kalvari mimi nimewekwa Huru,

Rumishael Ulomi

Copyright © www.kilicentric.com

R

Rumishael Ulomi

Author, Coach & Minister

Rumishael Ulomi is a seasoned leader and minister dedicated to integrating Christian values into leadership and life. He empowers individuals to reach their God-given potential through discipleship, coaching, and mentorship.

KiliCentric

The official blogof Rumishael Ulomi aka RyChris, hailing all the way from Moshi Kilimanjaro. .

Search This Blog

Labels

Follow Us

Should Your Religion Be Based On Your Feelings? Here is the answer..

Should a person decide what to believe based on his or her feelings or something that does not change with moods and circumstances? Big question! Imagine Jesus of Nazareth nailed up on the cross, dying for our sins. Suppose He said, “This is not fun. I am not feeling anything good up here. Let me off this cross. I expected good feelings, not this! Pain is not where it is at for Me. My commitment to die to pay the penalty for man’s sin is far beyond what I am feeling right now.” How would you have counseled Jesus when the bad pain hit Him? Feelings based religion is shaky. Commitments based on good feelings are subject to change any day. This unbiblical approach would make all our commitments very tentative, unpredictable, shaky. This includes: marriage, family, job and friends. A marriage vow would only mean, “I’ll stay with you as long as my good feelings last. I expect only good times, no bad ones.” Jesus did not bail out when the going got tough. Some beliefs a Christian should also...

The second necessary step in designing a successful nonprofit strategy is knowing your beneficiaries

Last week I started a series of blog posts on building a strong and successful strategy for your nonprofit and I started with mentioning the first necessary step you will need to examine before kicking off with your strategy. If you haven’t read that post, I recommend that you visit the article HERE before continuing with this one. Having familiarity with the first article will help you understand this one even much better. This week we are looking at the second step to take when designing your nonprofit strategy, and that step in designing and building a strong and successful strategy for your nonprofit is clearly knowing, stating, and understanding who your beneficiaries are. Some organizations talk about beneficiaries, others refer to participants, others to clients, service users or partners. Here we will refer to beneficiaries as the people whom your nonprofit seeks to benefit. The reason why many nonprofit strategies fail is because too often nonprofits and funders ignore the con...

Being set free by the master who holds the keys to life

After Jesus died on the cross He went down to hell, crushed the devil, and took the keys of life. The devil held us prisoners to fear of death, but now we are given the chance to enjoy eternal life with God the father. The greatest gift the human race can ever earn. It’s all free of charge to be set free, for the master has promised to do this free of charge to all those who desire to be free. If you have not yet accepted Christ, then you are still in a prison cell and you need to be freed from this. The only way that can happen is if you humble yourself and come to the master who has the keys to set you free. If you are in the devils prison, you can’t save yourself, not matter how good you think you are in escaping. You will never be able to escape until you let the master who took the keys set you free. You will try million ways and times, but I assure you, you will never succeed on your own. Many of you may say ‘well I am free’, I can assure you that you are only free in the flesh; ...

Join the Sikio Sikivu Diary

Get weekly leadership insights, biblical management tools, and discipleship resources delivered straight to your inbox.

No spam, just wisdom. Unsubscribe anytime.